banner

banner

Latest News

Powered by Blogger.
Thursday, August 31, 2017

RIPOTI MAARUMU KUHUSU FREEMASON NA JINSI YA KUJIUNGA NA JUMUHIYA HIYO

Ripoti Maarumu kuhusu Freemason Katibu wa Freemason Aeleza Yote:.....!

FREEMASONS NI NINI? Ni taasisi ambayo ilianzishwa miaka 350 iliyopita katika njia ambayo haikua rasmi ikaja kuhalalishwa miaka 300 iliyopita, hatujui vizuri ilianzishwa vipi ila inaaminika walikua wajenzi wanaojenga mashule, makanisa, wakati ule kulikua hakuna miji mikubwa kama sasa wala mahoteli, na wao walikua wakiishi pamoja na familia zao na wakihama wanahama pamoja, wakaanzisha miradi ya kujenga hoteli ndogo ndogo ili kusaidiana kama wajenzi na kujikwamua kiuchumi, wakawa wanafundishana.. yani kama una ujuzi unamsaidia na mwenzako kujua.
Anasema Katibu wa Freemason “Freemasons sio dini na tukikuta wewe ni mkristo tunakushinikiza ukristo wako, kama wewe ni mhindu unabaki kuwa mhindu, lakini freemasons orijino ilianzishwa na wakristo nchini Uingereza na baadae ikahamia Ulaya, Marekani, Australia na India Freemasons ikaja kuwa kubwa sana”

NCHI ZA AFRIKA AMBAZO FREEMASON NI KUBWA: Kwa nchi za Afrika Freemasons imekuja kuwa kubwa kwenye nchi kama za Nigeria na Ghana pia Sierra Leone, kwanza aliyewahi kuwa rais wa nchi hiyo Daudi Jawala alikua mmoja wetu. Freemasons ilianza mwaka 1646 alafu ikaja kuwa rasmi mwaka 1717 lakini kabla ya hapo katikati ilikua inafanywa kimya kimya.
KAZI ZINAZOFANYWA NA FREEMASON Kazi zinazofanywa sasa hivi na Freemasons ni kufundisha wanachama wake kuhusu majukumu yao kwa mwenyemwezi Mungu, kwa nchi yako, familia, na nchi unayofanyia kazi hata kama ni ugenini, na kutoa misaada.

WANACHAMA WA FREEMASONS DUNIANI: Duniani kote sasa hivi kuna wanachama milioni tatu laki tano wa freemasons na wanachangia dola za kimarekani zaidi ya milioni 400 kwa ajili ya misaada kila mwaka, yani kwa siku ni zaidi ya dola milioni moja kusaidia afya, elimu vilevile wajane wa wanachama wa freemasons wanasaidiwa ambapo pia ukiumwa na ukiwa na shida yeyote kuna msaada wa bure unapatiwa nakumbuka hata dr Charles Matwali alipoumwa sana, tulimpeleka uingereza kwa matibabu.

JINSI YA KUJIUNGA NA FREEMASONS: Ili kujiunga ni lazima uwe na umri wa miaka 21, ni hiari kujiunga na pia uwe unamwamini Mungu haijalishi ni Mungu gani, watu ambao hawamuamini Mungu hawaruhusiwi kuwa Freemasons, na lazima uwe mtu mkweli.
Ni lazima familia yako ikubali pia wewe kujiunga na freemasons kwa sababu freemasons hawatokubali kujiunga kwako kukufanye uwe masikini kutokana na kutoa misaada.
Unapotaka kujiunga ni lazima upeleke maombi yako kwa mtu unaemfahamu ambae yuko Freemasons, au kama hujui mtu Basi Piga Simu Namba 0652 720 339 baada ya hapo utapewa nakupewa taratibu za Malipo ya kufanya ili Uweze kujiunga, Baada ya kukamilisha Utaratibu freemasons itakupeleleza wewe na familia yako, na pia watakutembelea nyumbani kuongeana mkeo au mumeo au familia.
Inaweza kuchukua Wiki mbili kuruhusiwa kujiunga na freemasons baada ya kupeleka maombi, ambapo hapo ni kukubaliwa tu.

BAADA YA KUJIUNGA: Pia unatakiwa kujifunza vitu vingi na kuvihifadhi kichwani kama vile maneno ya kusema wakati unafanya ibada za freemasons kwa sababu tukiwa pamoja tunavyozungumzia sifa za kuwa binadamu kamili unaweza ukafananisha na ibada ya kanisani.

KUHUSU FREEMASON YA UINGEREZA:
Acha nizungumzie Freemason ya Uingereza ambayo mimi ni mmoja wao, Makao makuu yako London kwenye barabara inaitwa great queen street, Mkuu wa Freemasons Uingereza ni binamu yake malkia Elizabeth ambae tunamuita Grandmaster.
Kazi zote zinazofanyika na Freemasons zinaendeshwa kutoka kule, kwa mfano mv bukoba ilivyozama nilipiga simu kule kuomba msaada wakatuma pound elfu 10 ingawa na sisi hapa tuna kitengo chetu cha misaada ambayo kilichangia, maamuzi ya misaada mikubwa yanatoka Uingereza.
Kuna mahoteli ya freemasons Uingereza, Scotland na Ireland na katika nchi zilizokua za kisovieti zamani, tuna mahoteli duniani nzima ambapo kama upo kwenye freemasons ya Dar es salaam unaweza kuhudhuria vikao kwenye yeyote kati ya hizo hoteli duniani tunazomiliki ambazo zinatumika pia kama kumbi za mikutano yetu ili mradi wawe na uthibitisho kwamba wewe ni mmoja wetu.
Watu wengi huwa wanasema ni taasisi inayofanya mambo yake kwa siri lakini ukweli ni kwamba siri pekee iliyopo ni jinsi nitakavyokutambua kama wewe ni mmoja wetu, vingine vyote viko wazi na vinapatikana hata kwenye internet na unaweza kwenda kwenye maduka ya vitabu kote afrika mashariki hata uingereza ukapata nakala zote za freemasons ikiwemo hata maneno tunayosema tukifanya ibada zetu.
Kwa afrika Mashariki makao makuu ya freemasons yako Nairobi Kenya Kuna majumba 50 ya freemasons Afrika Mashariki Ingawa makao makuu yako Nairobi, jumba la Dar es salaam linajitegemea lenyewe na tunafanya miradi yetu na kusajili watu wetu hapahapa, hatuingiliwi na ofisi ya Nairobi, maamuzi yetu yanafanyika hapa hapa.

Hapa ni Freemasons Hall Dar es salaam ambapo Katibu wa freemason anasema kuna masonic lodge nne Dar es salaam.
FREEMASONS WANAPOKUTANA: Huwa tunakutana saa 12 jioni na kutoa ripoti ya tulivyovifanya tangu mkutano wa mwisho, kuhusu misaada tuliyotoa, wanachama wanaoumwa, na nani wa kwenda kumtembelea au kama kuna mwananchama mpya wa kumuapisha, kama hayupo tunajadiliana kuhusu mambo tofauti yanayotuhusu isipokua siasa na dini, tunakula pamoja na kila mtu anaondoka.

MNAKUTANA MARA NGAPI?
Inategemea kama tawi la Uingereza tulikua tunakutana mara mbili kwa mwaka, la huku Tanzania   tunakutana mara 11 kwa mwaka lakini siku hizi ni mara kumi, wengine wanakutana mara 5, inategemea na kazi za kufanya, mfano labda wanachama wa kuapisha ni wengi. Ibada inafanyikaje?

.
Ibada inaanza wakati vikao vinaanza, inahusisha mara nyingi kitu ambacho kinafanana na ibada kanisani, mara nyingi inahusika kumuweka mwananchama mpya kwenye mstari na mtazamo mmoja na aliowakuta na kwenye ibada huwezi kuvaa unavyotaka, lazima uvar suti na tai isipokua nchi kama India ambao hawavai tai.
Ukiwa mwanachama unapewa maswali ambayo ukiyajibu vizuri kwa muda wako unaweza kupandishwa cheo na inachukua muda kufikia degree ya tatu, tukiwa kwenye vikao mwenyekiti anaitwa Master na anao wasaidizi wawili, kwenye ibada mwenyekiti anakaa mashariki, msaidizi mmoja ana kaa mbele yake akimtizama na wa pili anakua anasaidia kwa shughuli nzima inayoendelea.
Kuna mwingine ambae ndio muongozaji wa sala na wakati tukisali, Mungu tunamuita Fundi mkuu aliyeumba sayari zote hiyo inahakikisha kwamba uwe Musilamu au mkristo tunakwenda sambamba.

ISHARA ZINAZOTUMIKA FREEMASONS
Alicho zungumza katibu wa Freemason
Kuna alama ya Compass inayotumika kuonyesha mwelekeo kwa mishale yake, kuna ruler na pembe nne ambavyo ni vitu vinavyotumika kwenye ujenzi ila vinaweza kutumika kufundisha kuhusu maisha, na ndio vinatumika hivyo wala sio kuhusu kitu kingine.
Tukifanya ibada zetu au kumkubali mtu kuingia freemasons lazima avae pajama au mavazi yanayotumika kulalia usiku, na haruhusiwi kuwa na pesa mfukoni, kuvaa saa au cheni ishara ya kuwa yeye ni masikini kama alivyozaliwa.
Uchawi, kuabudu shetani na mambo kama hayo watu wanayosema kwamba freemasons ndio inajihusisha na hivyo vitu ikiwemo kutoa uhai ndugu, ni waongo, hawana ujuzi wa kutosha, nakumbuka pia rais Moi aliunda kamati maalum kuchunguza uchawi na waabudu shetani na tuliitwa nikaenda kuwaeleza kwa muda wa karibu saa na nusu kuhusu freemasons, ingawa hawakuja kutupa ripoti kamili waliyopeleka kwa rais moi, walituambia kwamba wamekubali maelezo yetu na ingekua bora kama tungekua tunaeleza zaidi watu wajue na tusiwe wasiri.

RIPOTI YA CNN AUGUST 2010 KUHUSU FREEMASON:
Baadhi ya maseneta wa majimbo kadhaa ya Marekani walikiri kuwa ni wanachama wa Freemason ambapo ilifahamika kwamba Marais 12 waliowahi kuiongoza Marekani walikua wanachama wa Freemason ambapo pia watu 9 kati ya waliosaini hati ya uhuru wa Marekani walikua freemason akiwemo George Washington.
Appreciation  /   Boss Ngassa

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

5 comments:

  1. MALI,UTAJIRI AU FEDHA ZA NDAGU AU MAJINI KWA MUDA MFUPI MPAKA MASAA 72(SIKU 3) PAPO HAPO KWA MASHARTI MAALUM KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......

    KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA

    kwa maelezo kamili piga namba +255742162843

    (KWANINI USUMBUKE,HACHA KUTANGATANGA, NA MAISHA NI MAFUPI PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI (Tumia ufahamu kujinasuaUTAJIRI WA NDAGU(MASHARTI) NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......

    NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO
    (HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)
    MATIBABU MENGINEYO NI KAMA UTULIVU KATIKA NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE, KUONDOA MIKOSI, MABALAA, KUOSHA NYOTA, KUITAMBUA NYOTA YAKO NA ASILI YA KAZI YAKE, KAMA UNASUMBULIWA NA MAJINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI.

    NIPIGIE 0742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA.

    (kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
    1. uwe una umri wa miaka 18+
    2. uwe tayari kupokea masharti yote
    3.uwe na uwezo wa kutunza siri
    4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote
    KARIBU SANA KWA SHIDA NYINGINE PIA ULIYONAYO AMBAYO SIJATAJA INSHAALAH ITATATULIWA IKIWA NDANI YA UWEZO WANGU.

    ReplyDelete
  2. Naomba kujiunga Illuminati niwe tajiri

    ReplyDelete
  3. I want 2 b one of your member plz help

    ReplyDelete
  4. I want 2 b one of your member plz help me

    ReplyDelete

Item Reviewed: RIPOTI MAARUMU KUHUSU FREEMASON NA JINSI YA KUJIUNGA NA JUMUHIYA HIYO Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top