Kwa nyakati tofauti, viongozi hao wa kiroho wametajwa na wananchi kuwa wanajua siri za jamii hiyo kutokana na wao kuwahimiza kumtukuza na kushika mafundisho ya Mungu ambayo ndiyo kimbilio pekee la maisha ya hapa na mbinguni na siyo kuabudu mambo ya shetani.
Askofu wa Kanisa la Good News for All Nations lililo chini ya Huduma ya Rock Ministry lililopo Mbezi jijini Dar es Salaam, Diganyeka aliweka hadharani kwamba aliwahi kujiunga na Freemason na anasimulia jinsi alivyofanikiwa kujitoa katika taasisi hiyo kama ifuatavyo:
ALIVYOJIUNGA NA FREEMANSON
Alisema aliingia huko kupitia chama cha wanafunzi wa skauti na kuanza mafunzo ya kucheza kareti akiwa nchini kwao Kenya. Akiwa ndani ya chama hicho alipendwa na walimu wake na kuambiwa anafaa kuwa muumini wa dini hiyo inayozidi kupata umaarufu duniani.
AONESHWA CHUMBA CHA MAFUVU NA NYOKA
Baada ya kuonekana anafanya vyema katika medani ya michezo, alichaguliwa rasmi kuwa kiongozi wa wanafunzi hao na kupewa vazi lenye rangi nyekundu likiwa na nyota tano na kutunukiwa cheo cha heshima ya juu.
Alisema baada ya kupewa vazi hilo siku moja alichukuliwa na viongozi wa chama hicho na kwenda kufunguliwa chumba kimoja kilichokuwa kimejaa mafuvu ya binadamu kabla ya kuoneshwa kingine kilichokuwa na nyoka wakubwa.
KWA NINI ALIONESHWA VITU HIVYO
Askofu huyo alisimulia kuwa, lengo la kuoneshwa mafuvu na nyoka hao ni kuondoa hali ya hofu kila anapokutana na vitu hivyo kwani wakati mwingine huwekwa ndani ya nyumba kama mapambo.
Baada ya kuoneshwa vitu hivyo ndipo akapewa vazi hilo kama mtu mwenye heshima ndani ya chama cha skauti nchini Kenya.
SABABU ZA YEYE KUJITOA FREEMANSON
Alisema aliamua kujiondoa ndani ya taasisi hiyo baada ya kushindwa kukubaliana na masharti yake ambayo aliambiwa kutoa kafara mmoja wa ndugu zake wa karibu wakiwemo wazazi.
Alipogoma kutoa wazazi wake akaambiwa ajiweke dhamana mwenyewe ili siku akikiuka masharti umauti unamkuta. Alisema akiwa katika mabishano hayo ghafla alisikia sauti ndani ya moyo wake ikimtaka aende akahubiri Neno la Mungu, akatii.
Askofu Diganyeka alisema wapo watumishi wa Mungu ambao wamejiunga na taasisi hiyo na ili kuwatambua unatakiwa umakini wa hali ya juu. Alisema kuwa wengi wao hutumia alama ya kuvunja vidole na tendo hilo hufanyika kwa haraka.
Watumishi wengine huvaa pete za rangi mbalimbali ambazo nyuma yake zina nguvu ya mazingaombwe na kumfanya mtumishi aonekane anatumiwa na Mungu kumbe sivyo.
Alimaliza kwa kusema baadhi ya watumishi wa Mungu huvaa cheni za misalaba ambazo ukiziangalia kwa karibu huwa zina nembo ya Freemanson.
Naye Mtumishi wa Mungu kutoka Kenya ambaye yuko jijini Dar es Salaam anajulikana kama Mchungaji Joseph Kenya, amekuwa akizunguka vituo mbalimbali vya daladala jijini akihubiri habari za Mungu na kusema mambo anayoyaita ni siri za shetani za jamii hiyo.
Mtumishi huyu ambaye hajasema amejuaje siri hizo alishuhudiwa na mwandishi wetu akihubiri na kueleza aina ya nguo ambazo zimetengenezwa kuzimu na mtu akivaa huonekana moja kwa moja kwenye ramani ya kuzimu.
“Ipo mikanda yenye alama za Skull and Bones ambayo mtu akiivaa anapoteza nguvu za kiume au za kike,” alisema Mchungaji huyo huku akionesha mikanda hiyo.
Alisema kuwa hapa nchini kuna wahubiri wawili ambao hakuwataja majina huhubiri kupitia kwenye runinga huponya watu kwa nguvu za giza kupitia pete wanazovaa.
Ameliasa kanisa kuombea kazi ya Mungu kwa kuwa kuna watumishi wameingia katika kazi hiyo kama kondoo kumbe ni mbwa mwitu.
Aliwataka watu watoe mafungu yao ya kumi na sadaka, ili kazi ya Mungu izidi kuenea duniani na aliwaombea watu wenye mahitaji mbalimbali.
ASKOFU KAKOBE
Wachungaji na maaskofu wengine ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakipinga imani za kishetani ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospal Bible Fellowship, Zachary Kakobe ambaye hata dawa aliyokuwa akiitoa Mchungaji Ambilikile Mwasapile huko Loliondo alisema ni ya kishetani na akaifananisha na Deci.
“Niliwaambia kuwa yale ni mambo ya kishetani, wapinzani wakasema nawaonea wivu, sasa yamedhihirika. Hakuna dawa kubwa kama Yesu, mambo ya imani za kishetani ni chukizo kwa Mungu,” alionya Askofu Kakobe.
WAFUASI WA MZEE WA UPAKO
Mhubiri mmoja kutoka nchini Kenya, James Mbugua ambaye amekuwa akihubiri sehemu mbalimbali na kufanya kile kinachodaiwa kuwa ni kufichua siri za kundi la Freemasons, anadaiwa kujikuta katika msukosuko mkali maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam siku za nyuma baada ya kile kinachoelezwa kumhusisha Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ na Kundi la Freemasons.
Mkenya huyo alijikuta akianza kupigwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Mchungaji Lusekelo jambo lililomfanya akimbie bila viatu. Akizungumza na mwandishi wetu mtumishi huyo alikana kupigwa ila alikiri kuwa kuna kundi la watu lililotaka kumletea vurugu mitaa ya Kariakoo.
Gazeti hili lilizungumza na Mchungaji Lusekelo na kumuuliza juu ya hilo la waumini wake naye alisema: “Huenda ni kweli kwa kuwa watu mbalimbali hufika kanisani kwake kwa lengo la kuombewa na wengine hata hawajaokoka.”
MWINGIRA
Mtume na Nabii wa Kanisa la Efatha, Josephat Mwingira naye amekuwa akilaani mambo ya kishetani kanisani kwake katika mahubiri yake anayoyatoa katika makao makuu yake yaliyoko Mwenge jijini Dar es Salaam na aliwahi kumlaani Mchungaji Mwasapile kuwa tiba yake ni ya kishetani.
“Imeandikwa katika Biblia kwamba, ukipewa bure nawe toa bure. Iweje yeye anauza dawa hiyo, ikiwa Mungu amesema aponye watu…Hizi ni roho za kishetani zinazotaka kuwaangusha walio wengi ambao hawamjui Yesu Kristo kwani haiwezekani mtu atumiwe na Mungu halafu hata siku moja asimtaje Yesu,” alisema Mwingira.
Wachungaji wengine ambao hawaamini mambo au imani za kishetani na wamekuwa wakilaani mara kwa mara wale wote wanaoeneza mambo hayo ya shetani ni Mchungaji Getrude Lwakatare, Askofu wa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp Kadinali Pengo na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kianglikana nchini, Dk. Valentino Mokiwa.
Mawasiliano ya chama icho ni 0652 720 339
0 comments:
Post a Comment